http://esrf.or.tz/wp-content/uploads/2020/05/Capture.jpg

Organizer: Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-Idara ya Maarifa na Ubunifu

Event Date: 22-07-2017

Venue: Ukumbi wa Mikutano – ESRF

Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-Idara ya Maarifa na Ubunifu ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji Viumbe maji na Nyanda za malisho, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) – kikosi cha kambi ya Rwamkoma pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), inaandaa warsha ya siku moja kuhusu fursa za ufugaji samaki kibiashara kwa kutumia mabwawa, vizimba na matanki itakayofanyika tarehe 22/7/2017 siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa mikutano wa ESRF kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi.

Kutokana na tafiti zilizofanywa, imedhihirika kwamba, wananchi wengi wamekuwa na muitikio na hamasa ya ufugaji samaki kibiashara. Kwa kulitambua hilo ESRF ikishirikiana na taasisi zilizotajwa hapo juu, imeandaa mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wakufunzi waliobobea katika ufugaji wa samaki. Mada hizo zinajumuisha:-

 MADAMWASILISHAJITAASISI
1Ufugaji samaki katika mabwawa (pond fish farming),Emmanuel ManenoKituo Cha Ufugaji Samaki Mbegani – Idara Ya Ukuzaji Viumbe Majini
Nkhumbo Kantena (Mfugaji Kibiashara Mzoefu)
RUVU FARM
2Ufugaji  samaki katika vizimba (cage fish farming),Ltn. Kelvin NgondoJKT
3Ufugaji samaki katika matanki (Recirculating Aquaculture System-RAS)Ltn. Joseph LyakurwaJKT
4Uandaaji wa vyakula na malisho ya samakiDkt. Nazael MadallaSUA
5Masoko (Market Linkages)ESRFESRF

Watakaopenda kuhudhuria wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 21/7/2017 saa 5 asubuhi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba: 0626 645 245 au kujisajili kupitia