http://esrf.or.tz/wp-content/uploads/2020/05/Capture.jpg

Organizer: Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu

Event Date: 12-10-2016

Venue: Bariadi, Mkoani Simiyu

Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ikishirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu inaandaa Kongamano la Kitaifa la Vijana lenye kauli mbiu “Vijana na Viwanda kwa Mtazamo wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 “. Kongamano hili litafanyika tarehe 12 Oktoba 2016 Bariadi, Mkoani Simiyu. Washiriki wa Kongamano hili ni pamoja na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Wilaya, Wabunge, Wabunge kutoka kamati ya Bunge ya Biashara na Viwanda, Maafisa kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu, Maafisa wa Mkoa na Wilaya wa Vijana, Vijana kutoka Vyuo Vikuu, Asasi za Kiraia, Scout na Shirika la Maendeleo la Viwanda Vidogo (SIDO).