http://esrf.or.tz/wp-content/uploads/2020/05/Capture.jpg

Organizer: Taasisi ya Utafiti wa Kichumi na Kijamii (ESRF)

Event Date: 02-04-2016

Venue: Ukimbi wa Mikutano wa ESRF

Warsha Kuhusu Fursa Mpya za Kilimo Biashara

Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) inaanda warsha ya siku moja kuhusu fursa mpya za KILIMO BIASHARA itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 2/4/2016 katika ukumbi wa mikutano wa ESRF Mtaa wa Uporoto , Maeneo ya Victoria kuanzia saa tatu asubihi.

Kufuatia ESRF kushiriki katika kampeini ya Malkia wa Nguvu iliyoandaliawa na Clouds Media, kumekuwepo na muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi kutaka kufahamu zaidi kuhusu fursa zinazopatikana katika kilimo biashara.

Kwa kutambua hilo ESRF inaandaa Warsha hii kwa lengo la kutambulisha na kuelimisha zaidi wananch kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo zinapatikana katika sekta ya Kilimo.

Kutakuwa na mada mbalimbali zitakazotolewa na wakufunzi ambao wamebobea katika kilimo biashara. Maada zitakazotolewa ni pamoja na;

  • Shamba Kitalu (Green house)
  • Kilimo bila kutumia udongo (Hydroponic fodder & Vegetables)
  • Kilimo bila udongo na ufugaji samaki (Aquaponic)
  • Shamba Kitalu na Ujasiriamali (Green House & Entrepreneurship)
  • Azolla – chakula cha mifugo na mbolea
  • Ufugaji wa samaki katika mabwawa, matanki na vizimba (cages)
  • Ufugaji bora wa kuku

Watakaopenda kuhudhuria wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 2/4/2016 kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba: 0626 645 245 au barua pepe: mkilimo@esrf.or.tz