Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) wanasikitika kutangaza kifo cha mpendwa wetu Daktari Oswald Mashindano kilichotokea tarehe 27 Novemba 2024 Dar es Salaam.
Marehemu alijiunga na ESRF tarehe 01 Julai 2002 kama Mtafiti Mwandamizi na baadaye akahudumu katika wadhifa wa Mshauri Mwelekezi hadi umauti ulipomfika.
Daktari Mashindano anatarajiwa kuzikwa siku ya jumamosi tarehe 30 Novemba 2024 saa kumi jioni katika Makaburi ya Kinondoni.
Bwana Alitoa, Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe