Mwongozo wa Uwekezaji Mkoani Simiyu.

    Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Simiyu umeandaliwa sambamba na sera ya uwekezaji ya Tanzania. Unaainisha fursa za uwekezaji zinazopatikana katika mkoa wa Simiyu. Vile vile unaendana na dira ya mkoa wa Simiyu kama ilivyoelezwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli wa Tanzania mnamo tarehe 11, Januari 2017, na umeandaliwa kulingana na mifumo ya kimaendeleo ya kitaifa kama vile Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016-2021 (FYDP II).

    Mwongozo huu wa uwekezaji unatoa taarifa za uwekezaji kwa makampuni ya uwekezaji ya hapa nchini, ya nchi za nje na watu binafsi. Vile vile, Mwongozo unaainisha rasilimali na kubainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika mkoa wa Simiyu ili kuchochea biashara, maendeleo na ukuaji wa uchumi. Pia Mwongozo unadhamiria kukuza uwezo wa ushindani wa Mkoa wa Simiyu katika maeneo ambayo Mkoa una fursa za kiuchumi. Madhumuni mengine ni kukuza uwezo wa uzalishaji katika sekta muhimu za msingi ili kuleta maendeleo endelevu yatakayochangia kukua kwa pato la jumla la Taifa na ustawi wa mkoa wa Simiyu.

    Kwa hiyo, mkoa wa Simiyu na wilaya zake na Serikali za Mitaa: Bariadi, Busega, Itilima, Maswa, na Meatu wamedhamiria kutoa kipaumbele katika uwekezaji na kutoa huduma stahiki na motisha za kuvutia kwa wawekezaji katika Mkoa. Zaidi ya hayo, Ofisi ya Mkoa wa Simiyu na mamlaka zake za Serikali za Mitaa wataandaa mipango mwafaka na mazingira bora ya uendeshaji na ya kibiashara na watakuwa wanapatikana wakati wote ili kutoa maelezo zaidi kuhusu fursa zilizopo kwa wawekezaji wenye nia ya kuwekeza.

    Read MoreLatest Publications

View all


ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)