ESRF | E Brief
|
|
Kongamano la Kilimo Biashara Kanda ya Ziwa
Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP/UNEP inaandaa Kongamano la siku moja kuhusu KILIMO BIASHARA katika KANDA YA ZIWA litakalofanyika Jijini Mwanza siku ya Jumamosi tarehe 27/8/2016 katika Ukumbi wa ROCK CITY MALL ghorofa ya tatu kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi.
ESRF ilifanya utafiti na kisha kufanya majaribio katika wilaya sita na kubaini fursa nyingi katika sekta ya kilimo biashara hususani kilimo cha kisasa “smart farming”. Kwa kulitambua hilo ESRF ikishirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP/UNEP inaandaa Kongamano la kuelimisha wadau juu ya fursa zilizopo kwenye kilimo cha kisasa (smart farming)
Kutakuwa na MADA mbalimbali zitakazowasilishwa na wataalam na wadau waliofanikiwa katika Kilimo Biashara. Mada hizo zinajumuisha;
- Shamba Kitalu na Ujasiliamali (Green House & Entrepreneurship)
- Kilimo cha malisho ya mifugo (Hydroponic fodder)
- Kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo na ufugaji wa samaki (Hydroponic vegetable and Aquaponic)
- Ufugaji wa kisasa wa samaki katika vizimba, mabwawa na matanki (Cage, Pond and Circulative Fish Farming)
- Azolla - chakula cha mifugo na mbolea asilia
- Ufugaji wa kisasa wa nyuki
- Ufugaji bora wa kuku
Wanawake na vijana wanahimizwa kuhudhuria kwa wingi.
Watakaopenda kuhudhuria wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 26/8/2016 kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (sms) kupitia namba 0626645245 na 0627991530 au barua pepe kilimo@esrf.or.tz (Kongamano hili ni bure na washiriki watajigharimia gharama nyingine
Share it!
ESRF library has information and data on Economic, Social and Development issues. It is open to public from 8: am to 5: pm, Monday to Friday.
|
|
|